sw_tn/gen/23/10.md

52 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Sasa Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi
Hapa "Sasa" inatumika kuweka alama ya badiliko ya habari kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Efroni.
# Efroni
Hili ni jina la mwanamume.
# wana wa Hethi
Hapa "wana" ina maana ya wale ambao wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"
# alipowasikia wana wa Hethi
Nomino inayojitegemea "alipowasikia" inaweza kuwekwa kama "kusikia" au "kusikiliza". "ili kwamba wana wote wa Hethi waweze kumsikia" au "wakati wana wote wa Hethi walipokuwa wakimsikiliza"
# wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake
Hii inaelezea ni wana wapi wa Hethi walikuwa wakisikiliza. "wale wote waliokusanyika langoni mwa mji"
# langoni mwa mji wake
Lango la mji ilikuwa mahali ambapo viongozi wa mji walikutana kufanya maamuzi muhimu.
# mji wake
"mji ambao aliishi". Msemo huu unaonyesha ya kwamba Efroni alikuwa wa mji ule. Haimaanishi ya kwamba aliumiliki.
# bwana wangu
Huu msemo umetumika kuonyesha heshima kwa Abrahamu.
# mbele ya wana wa watu wangu
Hapa "mbele ya" ina maana ya watu waliokuwa kama mashahidi. "pamoja na wananchi kama mashahidi"
# wana wa watu wangu
Hii ina maana ya "wananchi wenzangu" au "Wahiti wenzangu"
# watu wangu
"watu wangu". Msemo huu unaonyesha ya kwamba efroni alikuwa sehemu ya kundi la watu. Haimaanishi ya kwamba alikuwa kiongozi wao.
# Ninakupatia uzike wafu wako
"Ninakupatia. Zika wafu wako"
# wafu wako
Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"