# Sasa Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi Hapa "Sasa" inatumika kuweka alama ya badiliko ya habari kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Efroni. # Efroni Hili ni jina la mwanamume. # wana wa Hethi Hapa "wana" ina maana ya wale ambao wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi" # alipowasikia wana wa Hethi Nomino inayojitegemea "alipowasikia" inaweza kuwekwa kama "kusikia" au "kusikiliza". "ili kwamba wana wote wa Hethi waweze kumsikia" au "wakati wana wote wa Hethi walipokuwa wakimsikiliza" # wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake Hii inaelezea ni wana wapi wa Hethi walikuwa wakisikiliza. "wale wote waliokusanyika langoni mwa mji" # langoni mwa mji wake Lango la mji ilikuwa mahali ambapo viongozi wa mji walikutana kufanya maamuzi muhimu. # mji wake "mji ambao aliishi". Msemo huu unaonyesha ya kwamba Efroni alikuwa wa mji ule. Haimaanishi ya kwamba aliumiliki. # bwana wangu Huu msemo umetumika kuonyesha heshima kwa Abrahamu. # mbele ya wana wa watu wangu Hapa "mbele ya" ina maana ya watu waliokuwa kama mashahidi. "pamoja na wananchi kama mashahidi" # wana wa watu wangu Hii ina maana ya "wananchi wenzangu" au "Wahiti wenzangu" # watu wangu "watu wangu". Msemo huu unaonyesha ya kwamba efroni alikuwa sehemu ya kundi la watu. Haimaanishi ya kwamba alikuwa kiongozi wao. # Ninakupatia uzike wafu wako "Ninakupatia. Zika wafu wako" # wafu wako Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"