sw_tn/gen/15/17.md

28 lines
969 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# tazama
Neno "tazama" hapa linatuamsha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.
# moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande
Mungu alifanya hivi kumuonyesha Abramu ya kuwa alikuwa akifanya agano na yeye.
# ilipita kati ya vile vipande
"ilipita katikati ya mistari miwili ya vipande vya wanyama"
# agano
Katika agano hili Mungu alimuahidi kumbariki Abramu, naye ataendelea kumbariki ikiwa Abramu ataendelea kumfuata yeye.
# Ninatoa nchi hii
Kwa kusema hivi, Mungu alikuwa akiwapa uzao wa Abramu nchi. Mungu alikuwa akifanya hivi, lakini uzao hawakuweza kwenda katika nchi hadi baada ya miaka mingi baadae.
# mto mkuu, Frati
"mto mkubwa, Frati". Hizi ni njia mbili zinazoelezea mto mmoja.
# Mkeni , Mkenizi, na Mkadmoni, Mhiti, Mperizi, Mrefai, Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.
Haya ni majina ya makundi ya watu ambao waliishi katika nchi. Mungu angeruhusu uzao wa Abrahamu kuwashinda watu hawa na kuchukua nchi yao.