# tazama Neno "tazama" hapa linatuamsha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata. # moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande Mungu alifanya hivi kumuonyesha Abramu ya kuwa alikuwa akifanya agano na yeye. # ilipita kati ya vile vipande "ilipita katikati ya mistari miwili ya vipande vya wanyama" # agano Katika agano hili Mungu alimuahidi kumbariki Abramu, naye ataendelea kumbariki ikiwa Abramu ataendelea kumfuata yeye. # Ninatoa nchi hii Kwa kusema hivi, Mungu alikuwa akiwapa uzao wa Abramu nchi. Mungu alikuwa akifanya hivi, lakini uzao hawakuweza kwenda katika nchi hadi baada ya miaka mingi baadae. # mto mkuu, Frati "mto mkubwa, Frati". Hizi ni njia mbili zinazoelezea mto mmoja. # Mkeni , Mkenizi, na Mkadmoni, Mhiti, Mperizi, Mrefai, Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi. Haya ni majina ya makundi ya watu ambao waliishi katika nchi. Mungu angeruhusu uzao wa Abrahamu kuwashinda watu hawa na kuchukua nchi yao.