sw_tn/gen/01/03.md

20 lines
698 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Na kuwe na nuru
Hii ni amri. Kwa kuamuru kuwepo na nuru, Mungu alifanya iwepo.
# Mungu akaona nuru, kuwa ni njema
"Mungu aliifikiria nuru na kufurahishwa nayo." Hapa "Njema" inamaanisha "kufurahisha" au "inayofaa."
# akaigawa nuru na giza
"alitenganisha nuru na giza" au "alifanya kuwepo na nuru wakati mmoja na giza wakati mwingine." Hii inamaanisha Mungu aliumba wakati wa mchana na usiku.
# Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza
Mungu alifanya vitu hivi katika siku ya kwanza ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.
# jioni na asubuhi
Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.