# Na kuwe na nuru Hii ni amri. Kwa kuamuru kuwepo na nuru, Mungu alifanya iwepo. # Mungu akaona nuru, kuwa ni njema "Mungu aliifikiria nuru na kufurahishwa nayo." Hapa "Njema" inamaanisha "kufurahisha" au "inayofaa." # akaigawa nuru na giza "alitenganisha nuru na giza" au "alifanya kuwepo na nuru wakati mmoja na giza wakati mwingine." Hii inamaanisha Mungu aliumba wakati wa mchana na usiku. # Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza Mungu alifanya vitu hivi katika siku ya kwanza ambapo ulimwengu ulianza kuwepo. # jioni na asubuhi Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.