sw_tn/deu/26/05.md

24 lines
687 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Musa anazungumza na Waisraeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" hapa ni katika umoja.
# Babu yangu alikuwa Mwaremi mzururaji
Huu ni mwanzo wa kauli ya kwamba mwanamume wa Kiisraeli anatakiwa kutengeneza anapoleta kikapu chake.
# Mwaremi mzururaji
Hii ina maana ya Yakobo, ambaye alikuwa baba wa Waisraeli wote. Aliishi miaka mingi katika Aramu-Nahairamu, eneo lililopo Shamu.
# na kukaa kule
"na kuishi maisha yake yote kule"
# Kule akawa
Neno "akawa" ni lugha nyingine kwa ajili ya "uzao wa Yakobo"
# kubwa, lenye nguvu
Maneno haya kimsingi yana maana moja. Yanasisitiza ya kwamba Israeli ikawa taifa kubwa na lenye nguvu. "kubwa sana"