sw_tn/act/12/20.md

44 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi
Luka anaendelea na simlizi nyingine juu ya maisha ya Herode.
# Sasa
Neno linaloweka daraja la kuelekea kwenye tukio jingine.
# Wakaenda kwa pamoja kwake.
Ni tukio lisilofurahisha kwamba wote walikwenda kwa Herode. "Wanaume waliowawakilisha watu wa Tiro na Sidoni walienda kwa pamoja kufanya mazungumzo pamoja na Herode.
# Wakawa na urafiki na Blasto
"Hawa watu walimfanya kuwa rafiki yao"
# Blasto
Blasto alikuwa msaidizi au ofisa wa Mfalme Herode.
# wakaomba amani,
"Wanaume wale waliomba kuwe na amani"
# nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme.
Yawezekana walinunua chakula hiki. "Watu wa Tiro na Sidoni walikuwa wakinunua chakula chao chote kutoka kwa watu waliotawaliwa na Herode."
# nchi yao ilipokea chakula
Inaonekana Herode alikuwa amezuia nchi yake kutoa chakula kwa Tiro na Sidoni kwasababu alikuwa amewakasirikia watu wa nchi hizo.
# Siku iliyokusudiwa
Hii inawezekana ilikuwa ni siku ambayo Herode alikubali kukutana na wawakilishi wa miji ya Tiro na Sidoni.
# mavazi ya kifalme
Mavazi ya gharama ambayo yangemdhihirisha kuwa alikuwa mfalme.
# kukaa kwenye kiti chake cha kifalme,
Hii ilikuwa ni kawaida ya Herode kufanya wakati watu walikuja kumwona.