# Sentensi unganishi Luka anaendelea na simlizi nyingine juu ya maisha ya Herode. # Sasa Neno linaloweka daraja la kuelekea kwenye tukio jingine. # Wakaenda kwa pamoja kwake. Ni tukio lisilofurahisha kwamba wote walikwenda kwa Herode. "Wanaume waliowawakilisha watu wa Tiro na Sidoni walienda kwa pamoja kufanya mazungumzo pamoja na Herode. # Wakawa na urafiki na Blasto "Hawa watu walimfanya kuwa rafiki yao" # Blasto Blasto alikuwa msaidizi au ofisa wa Mfalme Herode. # wakaomba amani, "Wanaume wale waliomba kuwe na amani" # nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme. Yawezekana walinunua chakula hiki. "Watu wa Tiro na Sidoni walikuwa wakinunua chakula chao chote kutoka kwa watu waliotawaliwa na Herode." # nchi yao ilipokea chakula Inaonekana Herode alikuwa amezuia nchi yake kutoa chakula kwa Tiro na Sidoni kwasababu alikuwa amewakasirikia watu wa nchi hizo. # Siku iliyokusudiwa Hii inawezekana ilikuwa ni siku ambayo Herode alikubali kukutana na wawakilishi wa miji ya Tiro na Sidoni. # mavazi ya kifalme Mavazi ya gharama ambayo yangemdhihirisha kuwa alikuwa mfalme. # kukaa kwenye kiti chake cha kifalme, Hii ilikuwa ni kawaida ya Herode kufanya wakati watu walikuja kumwona.