forked from WA-Catalog/sw_tn
32 lines
1.3 KiB
Markdown
32 lines
1.3 KiB
Markdown
|
# Sentensi Unganishi
|
||
|
|
||
|
Paulo anawasifu kwa huzuni yao ya ucha mungu, ari yao ya kutenda haki, na furaha ambayo ilimleta yeye na Tito.
|
||
|
|
||
|
# Habari za Jumla:
|
||
|
|
||
|
Hii inarejea kwenye barua ya kwanza ya Paulo kwa hawa waamini wa Wakorintho ambapo aliwakemea wakristo kukubali mtu kufanya zinaa na mke wa baba yake.
|
||
|
|
||
|
# wakati nilipoona waraka wangu
|
||
|
|
||
|
"wakati nilipojifunza waraka wangu"
|
||
|
|
||
|
# si kwa sababu mlikuwa na shida
|
||
|
|
||
|
Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa jinsi ya utendaji"siyokwa sababu kile nilichokisema katika barua yangu kiliwahizunisha ninyi"
|
||
|
|
||
|
# mliteseka si kwa hasara kwa sababu yetu
|
||
|
|
||
|
"mliteseka si kwa hasara kwa sababu tuliwakemea" Hii ina maa kuwa barua hiyo iliwasababishia huzuni, haukupita muda mrefu walifaidika kutokana na barua ile kwa sababu iliwaongoza kwenye toba
|
||
|
|
||
|
# Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu
|
||
|
|
||
|
Neno "toba" laweza kurudiwa kufafafnua uhusiano wake kwa kile kilichotangulia na kile kinachofuata.
|
||
|
|
||
|
# bila kujuta
|
||
|
|
||
|
Maana zaweza kuwa " Paulo hajuti kwamba amewasababishia huzuni kwa sababu huzuni hiyo iliwaongoza kwenye toba na wokovu) au Wakorintho hawatajuta kupitia huzuni kwa sababu inawaongoza kwenye toba yao na wokovu.
|
||
|
|
||
|
# Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti
|
||
|
|
||
|
Aina hii ya huzuni hupelekea kifo badala ya wokovu kwa sababu haileti toba
|