\v 8 Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria. \v 9 Kwa amri, "Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani," na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: "Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe." \v 10 Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.