sw_2sa_text_reg/13/37.txt

1 line
345 B
Plaintext
Raw Normal View History

\v 37 Lakini Absalomu akakimbia na kwenda kwa Talmai mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Mfalme akaomboleza kila siku kwa ajili ya mwanaye. \v 38 Hivyo Absalomu akakimbia na kwenda Geshuri na akakaa huko kwa miaka mitatu. \v 39 Moyo wa mfalme Daudi ukatamani kwenda kumwona Absalomu, kwa maana alikuwa amefarijika kwa habari ya kifo cha Amnoni.