sw_2sa_text_reg/13/10.txt

1 line
433 B
Plaintext
Raw Normal View History

\v 10 Amnoni akamwambia Tamari, "Lete chakula chumbani kwangu nikile katika mkono wako." Tamari akachukua mkate aliokuwa ameuandaa, na kuuleta katika chumba cha Amnoni kaka yake. \v 11 Alipoleta chakula kwake, Amnoni akamshikilia na kumwambia, "Njoo, ulale nami, dada yangu." \v 12 Yeye akamjibu, "Hapana, kaka yangu, usinilazimishe, kwani hakuna jambo kama hili linapaswa kufanyika katika Israeli. Usifanye jambo la aibu kiasi hiki!