Tue Apr 18 2023 20:17:32 GMT-0700 (Pacific Daylight Time)
This commit is contained in:
parent
f49c1f589a
commit
e280e744bf
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 6 \v 7 6 Israeli akawambia, "Kwa nini mlinitendea mimi vibaya hivyo kwa kumwambia mtu huyo kwamba mnaye ndugu mwingine?" 7 Wakasema, "Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?'Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?"
|
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 8 \v 9 \v 10 8 Yuda akamwambia Israeli baba yake, "Mtume kijana pamoja nami. Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu. 9 Mimi nitakuwa mdhamini wake. Utaniwajibisha mimi. Kama nisipomleta na kumweka mbele yako, basi nibebe lawama daima. 10 Kwani kama tusingekawia, bila shaka hata sasa tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili."
|
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 11 \v 12 11 Israeli baba yao akawambia, "Kama ni hivyo, basi fanyeni hivi. Chukueni baadhi ya mazao mazuri ya nchi katika mifuko yenu. Mchukulieni yule mtu zawadi: baadhi ya marhamu, asali, viungo na manemane, jozi na lozi. 12 Chukueni pesa mara mbili mikononi mwenu. Pesa iliyorudishwa katika magunia yenu, muichukue tena katika mikono yenu. Pengine walikosea.
|
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 13 \v 14 \v 15 13 Mchukueni ndugu yenu pia. Inukeni na mwende tena kwa mtu yule. 14 Mungu Mwenyezi na awape kuona rehema mbele ya huyo mtu, hivyo kwamba awafungulie ndugu yenu mwingine na Benjamini. Kama nikipotelewa na watoto, nimepotelewa." 15 Watu wale wakachukua zawadi hii, na katika mikono yao wakachukua mara mbili ya kiasi cha pesa, pamoja na Benjamini. Wakaamka na kushuka Misri na kusimama mbele ya Yusufu.
|
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 16 \v 17 16 Yusufu alipomwona Benjamini akiwa nao, akamwambia mtunzaji wa nyumba yake, "Walete watu hao ndani ya nyumba, chinja mnyama na umwandae, kwani watu hawa watakula chakula cha mchana pamoja nami." 17 Mtunzaji wa nyumba akafanya kama Yusufu alivyosema. Akawaleta wale watu nyumbani kwa Yusufu.
|
|
@ -0,0 +1 @@
|
|||
\v 18 \v 19 \v 20 18 Wale ndugu wakaogopa kwa vile walivyoletwa katika nyumba ya Yusufu. Wakasema, "Ni kwa sababu ya pesa iliyorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tulipoletwa ndani, kwamba atafute nafasi kinyume chetu. Kwamba aweze kutukamata na kutuchukua kama watumwa, na kuchukua punda wetu." Wakamsogelea mtunzaji wa nyumba ya Yusufu, 19 nao wakaongea naye mlangoni mwa nyumba, 20 wakisema, "Bwana wangu, tulikuja mara ya kwanza kununua chakula.
|
|
@ -0,0 +1,3 @@
|
|||
\v 21 \v 22 \v 23 21 Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu. 22 Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula. Hatujui aliyeziweka pesa katika magunia yetu." 23 Mtunzaji wa nyumba akasema, "Amani iwe kwenu, msiogope.
|
||||
Mungu wenu na Mungu wa baba yenu ndiye aliyeweka pesa katika magunia yenu. Nilipokea
|
||||
pesa yenu." Kisha mtunzaji wa nyumba akamleta Simoni kwao.
|
Loading…
Reference in New Issue