sw_tn_fork/rom/02/01.md

1.2 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo amesema kuwa wato wote ni wenye dhambi na anaendelea kuwakumbusha kuwa watu wote ni waovu.

Kwa hiyo umekosa sababu ya kujitetea

Neno "kwa hiyo" linaonyesha sehemu mpya ya barua. Inaonyesha suluhisho la sentensi ikionyesha yaliyosemwa "tangu Mungualipowaadhibu watu wanaoendelea kutenda dhambi, na hataonea huruma kwa sababu ya dhambi zao"

Wewe ni

Paulo haongei na mtu. Anajifanya kama Myahudi anayelumbana naye. Paulo anafanya haya kuwafundisha wasikilizaji wake kuwa Mungu atamhukumu kila mtu anayeendelea kutenda dhambi, awe Myahudi au wa Mataifa.

Wewe

Hapa neno "wewe" ni umoja.

Wewe mtu, wewe unayehukumu

Hapa neno "mtu" ilitumika kumdhihaki mtu aliyefikiri anaweza kufanya kama Mungu na kuwahukumu wengine. "Wewe ni binadamu tuu, lakini unawahukumu wengine na kusema kuwa wanastahili hukumu ya Mungu"

kwa unavyohukumu kwa wengine unahukumu kwako mwenyewe.

"Lakini unajihukumu mwenyewe kwa sababu unafanya mambo maovu kama wanavyofanya wengine"

Lakini twajua

Hii inajumuisha Wakristo walioamini na Wayahudi ambao sio Wakristo.

Hukumu ya Mungu ni kutokana na kweli ikiwaangukia wao

"Mungu atawahukumu watu kwa kweli na haki"

Wale wanaofanya mambo hayo

"watu wanaofanya mambo maovu"