sw_tn_fork/psa/108/001.md

29 lines
872 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Moyo wangu uko thabiti, Mungu
Hapa Daudi anajitambulisha kwa moyo wake. Pia, neno "thabiti" inamaanisha kuamini kabisa. "Moyo wangu uko thabiti kwako, Mungu" au "Nakuamini wewe kabisa, Mungu"
# Nitaimba sifa pia na moyo wangu uliotukuzwa
Hapa Daudi anajitambulisha kama kuwa na heshima ya kumsifu Mungu. "Unaniheshimu kwa kuniruhusu kukuimbia sifa"
# Amka, kinanda na kinubi
Hapa Daudi anaeleza kucheza vyombo kama kutembea kutoka usingizini. "Nitakusifu kwa kucheza kinanda na kinubi"
# Nitaamsha alfajiri
Hapa Daudi anaeleza alfajiri kuamka kama mtu kuamka asubuhi. "Nitakuwa nikikusifu alfajiri ifikapo"
# alfajiri
jua linapochomoza.