1.2 KiB
Mathayo 01 Maelezo ya Jumla
Muundo na upangiliaji
Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 1:23, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.
Dhana maalum katika sura hii
Nasaba
Nasaba ni orodha ambayo hurekodi mababu au wazao wa mtu. Orodha hizo zilikuwa muhimu sana katika kuamua nani aliyekuwa na haki ya kuwa mfalme, kwa sababu mamlaka ya mfalme mara nyingi ilipokelewa au kurithiwa kutoka kwa baba yake. Ilikuwa pia ya kawaida kwa mtu yeyote mashuhuri kuwa na kizazi cha kumbukumbu.
Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii
Matumizi ya sauti tulivu
Sauti tulivu hutumiwa kwa makusudi katika sura hii ili kuonyesha kwamba Yesu hakuzaliwa kupitia uhusiano wa ngono. Hapa, sauti tulivu inaashiria Roho Mtakatifu kama aliyetanguliza uja uzito wake Maria alipombeba mtoto Yesu. Kwa kuwa lugha nyingi hazina sauti tulivu, watafsiri wanapaswa kutafuta njia nyingine za kuwasilisha ukweli huo. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-activepassive)
Links:
| >>