sw_tn_fork/jdg/05/03.md

956 B

Taarifa za jumla:

wimbo wa Debora na Baraka kwa kutumia ushairi unaendelea.

Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi

Debora na Baraka wanazungumza na wafalme na viongozi kama vile wanawasikilizisha wimbo.

Ninyi wafalme ... ninyi viongozi

Hii inamaanisha wafalme na viongozi kwa ujumla, na sio viongozi au wafalme fulani.

wakati ulipotoka Seiri, ulipokwenda kutoka Edomu

Hii inarejea wakati ambao Waisraeli waliondoka Edomu na kuanza kuwateka watu wa Kanaani. Bwana aliwatia nguvu watu wake wakawashinda watu wa Kanaani.

Seiri

Huu ni mlima uliopo mpakani mwa Israeli na Edomu.

nchi ilitetemeka, na mbingu pia ilitetemeka; pia mawingu yalitoa maji.

Yaweza kuwa na maana ya 1) Hii ni lugha ya kishairi ambayo inasisitiza nguvu ya Bwana ambazo zina uwezo wa kusababisha tetemeko la ardhi au 2) watu wa Kanaani walianza kuogopa baada ya Waisraeli kutaka kuwavamia inafananishwa kama vile mbingu na nchi zinatetemeka.