forked from WA-Catalog/sw_tn
33 lines
1022 B
Markdown
33 lines
1022 B
Markdown
# Machozi yangu yamekuwa chakula changu
|
|
|
|
Mwandishi anazungumzia machozi yake kana kwamba ni chakula anachokula. Hii inamaanisha kuwa ana huzuni sana hadi hawezi kula. "Machozi yangu ni kama chakula changu na sili kitu kingine"
|
|
|
|
# mchana na usiku
|
|
|
|
Msemo huu unamaanisha siku nzima kwa kutaja mwanzo wake na mwisho wake. "siku nzima"
|
|
|
|
# adui zangu daima wanasema kwangu
|
|
|
|
Huku ni kukuza kwa neno. Adui zake hawasemi haya muda wote; wanasema mara kwa mara.
|
|
|
|
# Yuko wapi Mungu wako?
|
|
|
|
Adui wa mwandishi wanatumia swali hili kumkejeli na kuonesha kuwa hawaoni Mungu wake akimsaidia. "Mungu wako hayuko hapa kukusaidia"
|
|
|
|
# itisha akilini
|
|
|
|
Hii ni lahaja inayomaanisha kuwaza au kukumbuka kitu. "kumbuka"
|
|
|
|
# Ninamwaga nafsi yangu
|
|
|
|
Hapa neno "nafsi" inamaanisha hisia. Mwandishi anazungumzia nafsi yake kana kwamba ni kimiminiko anachomwaga. Msemo unamaanisha kuwa anaeleza uchungu wake wa hisia. "ninaeleza huzuni yangu"
|
|
|
|
# msongamano
|
|
|
|
"kundi la watu"
|
|
|
|
# furaha na sifa
|
|
|
|
Msemo huu unatumia maneno mawili tofauti kueleza wazo moja.
|
|
|