forked from WA-Catalog/sw_tn
33 lines
1.5 KiB
Markdown
33 lines
1.5 KiB
Markdown
# Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao
|
|
|
|
Hii ina maana ya kwamba Yusufu, ndugu zake, na Wamisri wengine wanakula katika sehemu tatu tofauti ndani ya chumba kimoja. "Watumishi walimhudumia Yusufu peke yake na ndugu zake peke yao na Wamisri, ambao walikuwa wakila naye, peke yao"
|
|
|
|
# Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao
|
|
|
|
Inawezekana hawa ni maafisa Wamisri wengine ambao walikula pamoja na Yusufu, lakini bado waliketi tofauti kutoka kwake na ndugu zake wa Kiebrania.
|
|
|
|
# kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri
|
|
|
|
Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Walifanya hivi kwa sababu Wamisri walidhani ilikuwa aibu kula pamoja na Waebrania"
|
|
|
|
# hawakuweza kula mkate
|
|
|
|
Hapa "mkate" ina maana ya chakula kwa ujumla.
|
|
|
|
# Wale ndugu wakakaa mbele yake
|
|
|
|
Inasemekana ya kwamba Yusufu alipanga ni wapi kila ndugu angeketi. Unaweza kuweka wazi taarifa iliyodokezwa. "Ndugu walikaa upande wa pili na yule mtu, kulingana na jinsi alivyopanga nafasi zao"
|
|
|
|
# mzaliwa wa kwanza kwa kulingana na haki yake ya uzaliwa, na mdogo kulingana na ujana wake
|
|
|
|
"mzaliwa wa kwanza" na "mdogo kuliko wote" inatumika pamoja kumaanisha ya kwamba ndugu wote walikaa kulingana na umri wao.
|
|
|
|
# Wale watu wakashangaa wote
|
|
|
|
"Hawa watu walishangazwa walipogundua hili"
|
|
|
|
# Lakini sehemu ya Benjamini ilikuwa mara tano zaidi ya kila ndugu zake
|
|
|
|
Msemo "mara tano" unaweza kuwekwa kwa ujumla zaidi. "Lakini Benyamini alipokea sehemu ambayo ilikuwa kubwa zaidi ya kile walichopokea ndugu zake"
|
|
|