sw_tw/bible/other/bridegroom.md

497 B

Bwana harusi

Ufafanuzi

Bwana harusi ni mtu anayemwoa bibi arusi katika sherehe ya harusi.

  • Katika utamaduni wa Kiyahudi nyakati za Biblia, sherehe iliwekwa siku ambayo bwana arusi alikuja kumchukua bibi harusi wake.
  • Katika Biblia, kwa kutumia tamathari ya semi, Yesu anaitwa "Bwana harusi" atakayetuijia siku moja "Bibi harusi wake," kanisa.
  • Yesu aliwafananisha thenashara na rafiki za Bwana harusi wanaosherehekea bwana harusi anapokuwa pamoja nao, lakini wanahuzunika anapoondoka.