1.2 KiB
1.2 KiB
Kuinama chini
Ufafanuzi
Kuinama maana yake kujikunja kwa unyenyekevu kuonesha heshima kwa mtu. "Kuinama chini" inamaanisha kupiga magoti chini sana, kwa kawaida uso na mikono ikielekea ardhini.
- Viashiria vingine ni pamoja na "kupiga goti" na "kuinamisha kichwa"( maana yake ni kuinamisha kichwa mbele kwa heshima ya unyenyekevu au katika huzuni).
- Kuinama chini pia kwaweza kuwa ishara ya mfadhaiko au maombolezo. Mtu "anayeinamishwa chini" amewekwa katika kiwango cha chini sana cha unyenyekevu.
- Kwa kawaida mtu atainama mbele ya mtu mwenye heshima ya juu kuliko yake au mwenye umuhimu mkubwa, kama wafalme na viongozi wengine.
- Kuinama mbele ya Mungu ni ishara ya kumwabudu.
- Katika Biblia, watu walimwinamia Yesu walipotambua kutokana na miujiza yake na mafundisho yake kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu.
- Biblia inasema kwamba Yesu atakaporudi, kila mtu atapiga goti kumwabudu.
Maoni ya Kutafasiri
- Kwa kutegemea na mazingira, neno hili laweza kutafasiriwa kwa neno au kifungu kinachomaanisha, "kuinamia" au "kuinamisha kichwa" au "piga goti".
- Neno "inama chini" laweza kutafasiriwa kama "Piga magoti" au "jinyenyekesha".
- Baadhi ya lugha zitakuwa na njia zaidi ya moja ya kutafasiri neno hili, kutegemea na mazingira.