sw_tw/bible/other/biblicaltimewatch.md

749 B

kukesha

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia, "kukesha" ulikuwa wakati wa usiku ambao katika huo mlinzi au mwangalizi wa mji alikuwa kazini akiangalia hatari yoyote kutoka kwa maadui.

  • Katika Agano la Kale, Waisraeli walikuwa na zamu tatu zikiitwa "mwanzo"( machweo hadi saa 4:00 usiku), "katikati" (saa 4:00 usiku hadi saa 8:00 usiku), na "asubuhi" (saa 8:00 hadi mawio).
  • Katika Agano Jipya, Wayahudi walifuata mfumo wa Kirumi na walikuwa na zamu nne, zikiitwa "ya kwanza" (machweo hadi saa 3 usiku) "pili" (3 usiku hadi saa 6 usiku), "tatu" (6 usiku hadi 9 usiku), na ya "nne" (saa 9 hadi mawio).
  • Hizi pia zaweza kutafasiriwa kwa vifungu vya jumla kama vile "jioni" au "katikati ya usiku" au "alfajiri," kutegemea na zamu inayotajwa.