sw_tw/bible/names/zerubbabel.md

457 B

Zerubabeli

Ufafanuzi

Zerubabeli lilikuwa jina la Waisraeli wawili katika Agano la Kale.

  • Mmoja wao alikuwa mzao wa Yehoyakimu na Sedakia.
  • Zerubabeli mwingine, mwana wa Shealitieli, alikuwa kiongozi wa kabila la Yuda wakati wa Ezra na Nehemia, Koreshi mfalme wa Uajemi alipowaacha huru Waisraeli kutoka katika utumwa wao huko Babeli.
  • Zerubabeli na Yoshua kuhani mkuu walikuwa miongoni mwa waliohusika kujenga upya hekalu na madhabahu ya Mungu.