sw_tw/bible/names/zedekiah.md

571 B

Sedekia

Ufafanuzi

Sedekia, mwana wa Yosia, alikuwa mfalme wa mwisho wa Yuda (597- 587 KK). Lakini pia kuna watu kadhaa katika Agano la Kale wenye jina Sedekia.

  • Mfalme Nebukadneza alimtawaza Sedekia kuwa mfalme wa Yuda baada ya kumteka Mfalme Yehoyakini na kwenda naye huko Babeli. Baadaye Sedekia aliasi jambo lililomfanya Nebukadneza kumkamata na kuuangamiza Yerusalemu.
  • Sedekia, mwana wa Kenaana, alikuwa nabii wa uongo wakati wa Mfalme Ahabu wa Israeli.
  • Mtu aliyeitwa Sedekia alikuwa mmojawapo wa wale waliosaini mkataba kwa Bwana nyakati za Nehemia.