sw_tw/bible/names/bethel.md

938 B

Betheli

Ufafanuzi

Betheli ulikuwa mji uliokuwa kaskazini mwa Yerusalemu katika nchi ya Kanaani. Hapo mwanzo uliitwa "Luzu."

  • Baada ya kupokea ahadi za Mungu kwa mara ya kwanza, Ibrahimu alimjengea Mungu madhabahu karibu na Betheli. Jina lake wakati huo halikuwa Betheli, lakini kwa kawaida ulirejerea kama "Betheli" uliokuwa unatambuliwa sana.
  • Wakati akikimbia kutoka kwa Esau nduguye, Yakobo alikaa usiku kucha karibu na mji huu na akalala pale nje juu ya ardhi. Alipokuwa amelala, aliota ndoto malaika wakipanda na kushuka mbinguni juu ya ngazi.
  • Mji huu haukuwa na jina hilo mpaka Yakobo alipouita hivyo. Kwa kuwa wazi zaidi, baadhi ya tafasiri zaweza kuiita Luzu "(baadaye ukaitwa Betheli)" katika kifungu kuhusu Ibrahimu, vilevile wakati Yakobo anafika pale kwa mara ya kwanza (kabla hajabadili jina lake).
  • Betheli imetajwa mara kwa mara katika Agano la Kale na ilikuwa sehemu ambapo matukio mengi mhimu yalitokea.