sw_tw/bible/names/beersheba.md

535 B

Beersheba

Ufafanuzi

Katika nyakati za Agano la Kale, Beersheba ulikuwa mji uliokuwa umbali wa maili 45 kusini magharibi mwa Yerusalemu katika eneo la jangwa ambalo kwa sasa linaitwa Negevu.

  • Jangwa lililouzunguka Beersheba lilikuwa ni eneo la nyika ambapo Hajiri na Ishmaeli walipotelea baada ya Ibrahimu kuwafukuza kutoka katika hema zake.
  • Jina la mji linamaanisha "kisima cha nadhiri." Ulipewa jina hili Ibrahimu walipoapa kwa kiapo kutokuwaadhibu watu wa Mfalme Abimeleki kwa kukatalia mojawapo ya visima vya Ibrahimu.