692 B
692 B
Babeli
Ufafanuzi
Babeli ulikuwa mji mkuu katika eneo lililoitwa Shinari kusini mwa Mesopotamia. Shinari ulikuja baadaye kuitwa Babiloni.
- Mji wa Babeli ulianzishwa na Nimrodi, mjukuu wa Hamu, aliyemiliki eneo la Shinari.
- Watu wa Shinari hatimaye wakawa na kiburi kwa kuamua kujenga mnara mrefu wa kuweza kufika mbinguni. Baada ulijulikana kama "Mnara wa Babeli."
- Kwa kuwa kwa kujenga mnara watu walikataa kutawanyika kama Mungu alivyokuwa ameagiza, yeye alichanganya lugha zao ili wasielewane. Hii iliwalazimisha kuondoka na kwenda kuishi maeneo mbalimbali ya dunia.
- Kiini cha maana ya neno "Babeli" ni "machafuko," likitokana na wakati Mungu alipochanganya lugha ya watu.