sw_tw/bible/kt/bond.md

1.3 KiB

funga

Ufafanuzi

Neno "funga" linamaanisha kukaza kitu kwa usalama. Kitu kilichofungwa au kuunganishwa pamoja kinaitwa "muungano". Neno "kufunga" ni sehemu ya neno hili katika wakati uliopita.

  • "Kufungwa" inamaanisha kufunga au kuzonga katika kitu kingine.
  • Katika hali ya tamathari, mtu anaweza "kufungwa" katika nadhiri, kumaanisha "analazimika kutimiza" alichokiahidi.
  • Neno "vifungo" linamaanisha chochote kinachofunga, "weka pamoja, au kumweka mtu gerezani. Kwa kawaida inamaanisha vifungo vya kimwili, pingu au kamba zinazomfanya mtu asiwe huru kuondoka alipo.
  • Katika nyakati za Biblia, vifungo kama vile kamba au minyororo ilitumika kumfunga mfungwa katika ukuta au chini ya jiwe la gereza.
  • Neno "funga" laweza pia kutumika kuzungumzia kufunga kidonda kwa kitambaa ili kukisaidia kupona.
  • Mfu aweza "kuzongwa" kwa sanda katika maandalio ya mazishi.
  • Neno "kifungo" hutumika kitamathari kurejerea kitu fulani, kama vile dhambi, inayomwongoza au kumfanya mtumwa.
  • Kifungu chaweza kuwa uhusiano wa karibu kati ya watu ambao wanasaidiana kihisia, kiroho na kimwili. Hii inatumika katika kifungo cha ndoa.
  • Kwa mfano, mwanamke na mwanamme "wamefunwa" au "kuunganishwa. Ni kifungo ambacho Mungu hapendi kivunjike.

Maoni ya Tafasiri

Neno "funga" laweza pia kutafasiriwa kama "kaza" au "zungushia"