sw_tw/bible/kt/bless.md

1.8 KiB

Kubariki

Ufafanuzi

"kubariki" mtu au kitu maana yake ni kusababisha mema na mambo ya manufaa kufanyika kwa mtu au kitu kinachobarikiwa.

  • Kumbariki mtu pia inamaanisha kuonesha nia chanya na vitu vyenye manufaa kumpata mtu huyo.
  • Katika nyakati za Biblia, kwa kawaida baba alitamka baraka maalumu kwa wanawe.
  • Watu "wanapombariki" Mungu au kuonesha hamu ya kuwa Mungu abarikiwe, inamaanisha wanamwinua.
  • Neno "baraka" wakati mwingine linatumika kwa kukitakasa chakula kabla hakijaliwa, au kwa kumshukuru na kumsifu Mungu kwa ajili ya chakula.

//kutokana na maoni hapa chini: Ni mhimu kutoa maana, lengo, au kuzingatia matumizi ya mzizi wa neno "bariki" ambalo kimsingi linapendekea kustawi au kuwa na wingi wa vitu au utajiri. Kwa kuzingatia wingi wa mafundisho ya kimaandiko juu ya upendo wa Mungu, rehema na neema ambayo siyo ya kale tu bali hata sasa. Kwa kuzingatia uangalizi, ulinzi, na uwepo wa Roho wa Mungu. Na kwa ajili yetu kumbariki Mungu, kwa kutoa shukurani, kuthamini, na kuelewa kama tunavyojifunza na kumfuata(kumtii)//

Maoni ya Kutafasiri

  • "Kubariki" kwaweza kutafasiriwa kama "kuandaa kwa wingi" au "kuwa mwema ."
  • "Mungu ameleta baraka kuu" ifasiriwe kama "Mungu ametoa mambo mengi mema kwa" au "Mungu ametoa kwa wingi kwa ajiri" au "Mungu amesababisha Mambo mema kutokea kwa".
  • "Amebarikiwa" ifasiriwe kama "atanufaika sana" au "atapitia mambo mema" au "Mungu atamfanya kustawi".
  • "Amebarikiwa mtu yule" yaweza kutafasiriwa kama "Ni vema kiasi gani kwa mtu ambaye".
  • Vioneshi kama vile, "abarikiwe Bwana" yaweza kutafasiriwa kama, "na asifiwe Bwana" au "Bwana asifiwe" au "Ninamtukuza Bwana".
  • Katika mazingira ya kubariki chakula, hii yaweza kutafasiriwa kama, "alimshukuru Mungu kwa ajili ya chakula" au "alimshukuru Mungu kwa kuwapa chakula" au "alikitakasa chakula kwa kumsifu Mungu.