sw_tn/rom/14/intro.md

1.1 KiB

Warumi 14 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivi kwa mstari wa 11 wa sura hii, ambayo Paulo ananukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Dhaifu katika imani

Paulo anafundisha kwamba Wakristo wanaweza kuwa na imani ya kweli na wakati huo huo kuwa "dhaifu katika imani" katika hali fulani. Hii inaelezea Wakristo ambao imani yao ni changa, haina nguvu, au haijaeleweka.(See: rc://*/tw/dict/bible/kt/faith)

Vikwazo vya chakula

Dini nyingi katika inchi ya kale ya Mashiriki ya Karibu zilizuia kile kilicholiwa. Wakristo wana uhuru wa kula kile wanachotaka. Lakini wanahitaji kutumia uhuru huu kwa hekima, kwa namna ambayo huheshimu Bwana na haisababishi wengine kutenda dhambi. ((See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin))

Kiti cha hukumu cha Mungu

Kiti cha hukumu cha Mungu au Kristo kinamaanisha wakati ambapo watu wote, ikiwa ni pamoja na Wakristo, watahukumiwa kwa jinsi walivyoishi maisha yao.

<< | >>