sw_tn/rom/02/25.md

1005 B

Maelezo yanayounganisha:

Paulo anaendelea kuonyesha kwamba Mungu, kwa sheria zake, anawaadhibu hata Wayahudi ambao wana sheria za Mungu.

Kwa kuwa tohana imekupa faida wewe

"Nasema haya yote kwa sababu kutahiriwa kumekupa faida"

Kama ukiwa mkiukaji wa sheria

"Kama usipotii amri zilizopo katika sheria"

Kutahiriwa kwako kutakuwa kutokutahiriwa

Hii inamfananisha Myahudi asiyetii sheria na mtu ambaye ametahiriwa lakini anaonekana kama hajatahiriwa : anaweza kuwa Myahudi lakini akaishi kama mtu wa Mataifa. "Ni kama vile haujatahiriwa"

Mtu asiyetahiriwa

"Mtu ambaye hajatahiriwa"

Kuyashika maagizo ya sheria

"kutii kilichoamriwa kwenye sheria"

kutokutahiriwa kwake hakuwezi kuchukuliwa kama kutahiriwa? Na ambaye hajatahiriwa kwa asili hawezi kukuhukumu... sheria?

Paulo aliuliza maswali mawili kusisitiza kuwa kutahiriwa sio jambo la kumfanya mtu kuwa na haki mbele za Mungu. "Mungu atamchukulia kama mtu aliyetahiriwa.... na mtu ambaye hajatahiriwa ... atakuhukumu... sheria."