sw_tn/rev/12/intro.md

1.5 KiB

Ufunuo 12 maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Wasomi wengi wanaamini kwamba matukio ya sura hii ni ya kipindi kilichopita na kipindi kijacho. Mwandishi anaweza zungumzia matukio bila kusema ni kipindi gani yalitokea. Hata hivyo, Yohana anayazungumzia matukio haya kana kwamba ndio yanakaribia kutokea.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo mshororo wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 12:10-12

Dhana muhimu katika sura hii

Nyoka

Kuashiria Shetani kama nyoka inakusudiwa kumfanya msomaji kukumbuka hadithi ya majaribu katika Bustani la Edeni. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

Mwanamke ametajwa katika mifano nyingi lakini utambulisho wake hauko wazi.Sura hii inazungumzia pia kuhusu kutokea kwa mpinga Kristu. (Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]] na [[rc:///tw/dict/bible/kt/antichrist]])

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Ishara kuu ilionekana mbinguni"

Haieleweki iwapo hii ilionekana kwa kila mtu duniani ama ilionekana tu na Yohana katika maono yake. Mtafsiri atakuwa na utata iwapo swala hili haliko wazi. Kwa kiingereza hii hufanyika kutumia sauti ya kupita ingawa siyo kila lugha ina uwezo huu.(Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-activepassive]] na [[rc:///ta/man/translate/writing-apocalypticwriting]])

<< | >>