sw_tn/mrk/03/intro.md

2.0 KiB

Marko 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Sabato

Ilikuwa kinyume cha sheria ya Musa kufanya kazi siku ya sabato. Mafarisayo waliamini kumponya mtu mgonjwa siku ya Sabato ilikuwa "kazi," hivyo wakasema kwamba Yesu alifanya makosa wakati alimponya mtu siku ya Sabato. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/lawofmoses)

"Kukufuru dhidi ya Roho"

Hakuna mtu anayejua kwa hakika hatua ambazo watu hufanya au maneno gani wanayosema wanapotenda dhambi hii. Hata hivyo, labda wao humtusi Roho Mtakatifu na kazi yake. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwafanya watu kuelewa kuwa wao ni wenye dhambi na wanahitaji kusamehewa na Mungu. Kwa hiyo, yeyote asiyejaribu kuacha dhambi huenda anakufuru Roho. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/blasphemy]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/holyspirit]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanafunzi kumi na wawili

Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili:

Katika Mathayo:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomeo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Tadayo, Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.

Katika Marko:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambao aliwaita Boanerge, yaani, wana wa ngurumo), Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Tadayo Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.

Katika Luka:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Simoni (aitwaye Zeloti), Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Isikariote.

Thadayo labda ni Yuda, mwana wa Yakobo.

Ndugu na Dada

Watu wengi huwaita wale ambao wana wazazi sawa "ndugu" na "dada" na kuwafikiria kama watu muhimu zaidi katika maisha yao. Watu wengi pia huita wale walio na babu na nyanya sawa "ndugu" na "dada." Katika sura hii Yesu anasema kwamba watu muhimu zaidi kwake ni wale wanaomtii Mungu. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/brother)

<< | >>