sw_tn/luk/07/29.md

973 B

Taarifa kwa Ujumla

Luka, mwandishi wa kitabu, alichangia juu ya mwitikio wa watu kwa Yohana na Yesu.

Wakati watu wote ... ubatizo wa Yohana

Mstari huu unaweza kurekebishwa wazi zaidi. NI: "wakati watu wote waliokuwa wamebatizwa na Yohana, wakiwemo watoza ushuru, walisikia hiki, wakatangaza kwamba Mungu ni mwenye haki.

walitangaza kuwa Mungu ni mwenye haki

"Walisema kwamba Mungu amejionyesha mwenyewe kuwa ni mwenye haki" au "walitangaza kuwa Mungu alitenda kwa haki

sababu walibatizwa na ubatizo wa Yohana

Hii inaweza ikasemwa katika kauli tendaji NI: "sababu walikubali Yohana awabatize" au "sababu Yohana aliwabatiza wao."

walikataa kusudi la Mungu kwa ajili yao wenyewe

"walikataa ambacho Mungu alitaka wao wafanye" au "chagua kutotii ambacho Mungu aliwaambia"

wao hawakubatizwa na Yohana

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji NI: "ambao Yohana hakuwabatiza" au "ambao walikataa kubatizwa na Yohana" au " wale waliokataa ubatizo wa Yohana."