sw_tn/luk/07/11.md

1.3 KiB

Sentensi Unganishi

Yesu anaenda katika mji wa Naini, pale alipomponya mtu aliyekuwa amekufa.

Naini

ni jina la Mji

tazama, mtu aliyekufa alikuwa kafa

Neno "Tazama" linatuashiria utangulizi wa simulizi ya mtu aliyekufa kwenye habari. Lugha yako inaweza kuwa na njia ya kufanya hivi. NI: "Kulikuwa na mtu aliyekufa"

mtu ambaye alikuwa amekufa alikuwa kabebwa

Hii inaweza ikasemwa katika kauli tendaji. NI: watu walikuwa wanapeleka nje ya mji mtu aliyekufa"

mwana pekee wa mama yake (ambaye alikuwa mjane)

"alikuwa mwana pekee wa mamaye, na alikuwa mjane" Hii ni taarifa iliyotangulia kuhusu aliyekufa na mama yake.

ilitokea kuwa

hii sentensi inatumika hapa kuonyesha mwanzo wa habari mpya. kama Lugha yako ina njia nyingine ya kufanya hivi unaweza kutumia hapa.

mjane

mwanamke ambaye mumewe amesha kufa

alisukumwa na huruma kwa ajili yake

"aliona huruma kwa ajili yake"

akaja mbele

"akaenda mbele" au "akamsogelea aliyekufa"

jeneza lililokuwa limebeba mwili

Hiyo ilikuwa ni machela au kitanda kilitumika kubeba mwili kwenda maeneo ya kuzika. kisingeweza kuwa kitu cha kuzikia. Tafsiri nyingine inapunguza uthamani "Jeneza" au "Kiti cha msiba"

nasema kwako

Yesu alisema hili kuonyesha mamlaka yake "Nisikilize!"

maiti

mtu alikuwa bado amekufa; sasa alikuwa hai. Itakuwa lazima kusema hili wazi. NI: "ni mtu aliyekuwa amekufa."