sw_tn/lev/26/25.md

1.3 KiB

Nitaleta upanga juu yenu

Hapa "upanga" huwakilisha jeshi au shambulizi kutoka kwa jeshi. : "Nitaleta jeshi la adui dhidi yenu" au "nitasababisha jeshi la adui kuwavamia nyinyi"

utakaowaadhibu kwa kisasi

"amabao utawaadhibu nyinyi"

kwa sababu ya kulivunja agano

"kwa kutotii agano" au "kwa sababu hamlitii agano"

Nanyi mtakusanywa pamoja

Hii yaweza kutamkwa katika mtingo wa utendaji. : "Mtakusanyika pamoja" au "Mtajificha"

nanyi mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu

Hapa " mikononi" humaanisha "kwenye udhibiti" na humaanisha kushindwa na adui. Hii yaweza kutamkwa katika mtindo wa utendaji. : "adui zenu watawashindeni"

Nitakapokomesha mgao wa chakula,

Kule kukiharibu chakula ambacho watu wamikitunza au kuwafanya watu wasikipate kumezungumziwa kana kwamba kukata uwaji wa chakula. : "Nitakapoharibu chakula mlichokihifadhi" au "Nitakapowazuia msiweze kupata chakula"

wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako kwenye chombo kimoja cha kuokea

Hii hudokeza kwamba kutakuwa na unga kidogo sana kiasi kwamba chombo kidogo sana cha kuokea kitaweza kubeba mikate yote ambayo wanawake wengi wateza kuweka ndani yake.

watakugawia mkate wako kwa uzani

Hii humaanisha kwamba kutakuwa na chakula kidogo sana watatakiwa kukipima ni kiasi gani kila mtu anapata.