sw_tn/jos/07/08.md

1.2 KiB

Maelezo ya jumla

Yoshua anamwelezea Mungu juu ya wasiwasi uliokuwepo

niseme nini, baada ya Israeli kuwatega migongo maadui zao!

Yoshua aliyasema haya kuonesha jinsi alivyokuwa amekatishwa tamaa kana kwamba alikuwa hana hata neno la kusema. "Sijui kitu cha kusema.Israeli imegeuka na kukimbia mbele za adui zao."

Israeli kuwatega migongo maadui zao

Kufanya hivyo kunamaanisha kukimbia kutoka kwa maadui zao. "Israeli imekimbia kutoka kwa maadui zao."

watatuzunguka na kuwafanya watu wa nchi kulisahau jina letu

Kuwafanya watu wasahau jina la Israeli ina maana ya kuwafanya waasahau Waisraeli. Kwa namna hii watalifanya hili kwa kuwaua Waisraeli. "Watatuzunguka na kutuua, na watu wa dunia watatusahau sisi."

Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?

Kifungu cha maneno "jina lako kuu" mahali hapa kina maana ya Sifa za Mungu na uweza. "Na je utafanya nini ili watu wajue kuwa wewe ni mkuu."

Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?

Yoshua alitumia swali hili kwa ajili ya kumtahadharisha Mungu kwamba kama Waisraeli watauwawa, ndipo watu wengine watadhani kuwa Mungu si mkuu. "Hakutakuwa na kitu utakachokifanya kwa ajili ya jina lako kuu" au "Watu hawatajua kwamba wewe ni mkuu."