sw_tn/ezk/34/01.md

897 B

neno la Yahwe likaja

"Yahwe akanena neno lake."

wachungaji wa Israeli

Hili neno linawalinganisha viongozi wa Israeli ambao wanaotakiwa kuangalia watu wao pamoja na wachungaji ambao wanaotakiwa kuangalia kundi lao. "viongozi wa Israeli walio kama kondoo"

Tabiri na sema

Tazama tafsiri yake katika sura ya 21:8.

wanajichunga wenyewe

"wanajilisha na kujichunga wenyewe."

Je! wachungaji hawapaswi kulilinda kundi?

Yahwe anatumia hili swali kuwakaripia viongozi kwa kuacha kuwaangalia watu.

Mnakula mafungu yaliyonona

Inaonyesha kwamba fungu lililonona hutoka kwenye kondoo na mbuzi. "Mnakula sehemu za kondoo na mbuzi zilizonona"

mnavaa sufu

"vaa sufu kutoka kondoo"

Mnachinja walionona

"Mnachinja mifugo wanene ili muweze kuwala"

wanene

"kondoo mwenye afya na mbuzi" au "kondoo na mbuzi walio nona kabia"

hamkuwalisha siku zote

"msiwalishe na kulichunga kundi"