sw_tn/ezk/04/01.md

1.2 KiB

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaendelea kunena na Ezekieli. Anamwambia Ezekieli kuchukua tofali na udongo na vipande vya mbao na kutenda kana kwamba alikuwa Yahwe akiuharibu mji wa Yerusalemu.

mwanadamu

"mwana wa mwanadamu" Mungu anamwita Ezekieli hivi kusisitiza kwamba Ezekieli ni mwanadamu tu. Mungu ananguvu na anaishi milele, lakini watu hawaishi milele.

chonga mji wa Yerusalemu

"chonga picha ya mji wa Yerusalemu"

laza ngome juu yake

"zunguka mji ili kuunyakua"

jenga ngome juu yake

"jenga kuta juu yake." "Kuta zitawahifadhi watu wasiuache mji.

Anza kushambulia juu yake

"jenga hanamu nje ya hiyo kwa ajili ya maadui kuingia ndani." Yerusalemu ilikuwa na ukuta kuizunguka kuwalinda watu ndani.

Weka shambulio la ghasia kuizunguka

"Shambulio la ghasia" ni miti mikubwa au nguzo ambazo watu katika vita wangechukua na kupiga juu ya ukuta au mlango hivyo wangeuangusha chini na kuingia ndani. "Weka kuizunguka nguzo kubwa watu watumie kuvunja malango na kuingia ndani"

weka uso wako juu yake

"itazame kwa uso wa hasira"

nyumba ya Israeli

Neno "nyumba" ni mfano wa familia iishiyo katika nyumba, katika kesi hii Waisraeli, uzao wa yakobo zaidi ya miaka mingi.