sw_tn/ezk/01/04.md

1.3 KiB

Sentensi Unganishi:

Ezekieli anaendelea kuelezea ono lake.

upepo wa dhoruba

Hii ni dhoruba ambayo yenye upepo mwingi.

unakuja kutoka kaskazini

Kaskazini ni uelekeo wa mkono wako wakati utazamapo jua linapokuwa linachomoza.

wingu kubwa lenye moto ndani yake

Hili linaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya: "Hii dhoruba ilikuwa kubwa pamoja na moto ukiwaka ndani yake"

moto ukiwaka

Maana ziwezekanazo 1) "mwanga ukiwaka" au 2) ukiwaka wakati wote."

na nuru ndani yake na kung'aa ukizunguka ndani yake

"na nuru kali sana ikimulika ilikuwa imelizunguka wingu ndani yake".

rangi ya kaharabu

"njano inayong'aa kama kaharabu" au "njano inayong'aa"

kaharabu

utomvu wa njano ngumu ambayo ilitumika kama pambo zuri juu ya kito

Katikati

"katikati ya dhoruba"

ulikuwa kama mwonekano wa viumbe hai vinne

"kulikuwa na vitu ambavyo vilifanana kama viumbe vinne"

Huu ulikuwa mwonekano wao

"Hivi ndivyo ambayo viumbe vinne vilivyokuwa vikionekana"

vilikuwa vikifanana na mtu

"vile viumbe vinne vilifanana na watu"

lakini vilikuwa na sura nne kila mmoja, na kila kiumbe kilikuwa na mabawa manne

"lakini kila kiumbe kilikuwa na sura tofauti tofauti na mabawa manne." Kila kiumbe kilikuwa na uso mmoja kwa mbele, uso mmoja upande wa nyuma, na uso mmoja kwa kila upande wa kichwa chake.