sw_tn/deu/23/21.md

976 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "kwako" na "wako" hapa ni katika umoja.

haupaswi kukawia kuikamilisha

"hautakiwi kutumia muda mrefu kukamilisha kiapo hiki"

maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho

"kwa sababu Yahwe Mungu wako atakulaumu na kukuadhibu iwapo hautakamilisha kiapo chako"

Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako

Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Lakini, kama hautatoa kiapo, hautakuwa umetenda dhambi kwa sababu hautakuwa na kiapo cha kutimiza"

Kile ambacho kimetoka kinywani mwako

Hii ni lahaja. "Maneno uliyozungumza"

kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako

"chochote ulichoapa kwa Yahwe Mungu wako ambacho utafanya"

chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako

"chochote ambacho watu wamesikia ukiahidi kufanya kwa sababu ulitaka kukifanya"

kinywa chako

"ili kwamba watu wasikie ukikitamka"