sw_tn/deu/21/13.md

919 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba alikuwa akizungumza na mtu mmoja, kwa hiyo maneno "zako" na "yako" ni katika umoja.

atazivua nguo alizokuwa amezivaa

Atafanya hivi baada ya mwanamume kumleta katika nyumba yake na atakaponyoa nywele na kukata kucha kama zilivyotajwa katika 21:10. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "atazivua nguo zake za watu wake na kuvaa nguo za Kiisraeli"

wakati alipochukuliwa mateka

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ulipomchukua mateka"

mwezi mzima

"mwezi mzima kamili" au "mwezi kamili"

Lakini usipofurahishwa naye

Unaweza kufanya hivi kuwa wazi ya kwamba mwanamume alilala na mwanamke. "Lakini ukilala naye na kisha kuamua ya kwamba haumtaki kama mkeo"

kumruhusu aondoke apendaye yeye

"mruhusu aondoke atakapo yeye"

kwa sababu umemdhalilisha

"kwa sababu umemuabisha kwa kulala naye na kisha kumfukuza"