sw_tn/deu/21/08.md

965 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuwaambia viongozi kile wanachopaswa kusema watakapoosha mikono yao juu ya mtamba. Anazungumza nao kana kwamba anazungumza na mtu mmoja, kwa hiyo maneno "wako" na "kwao" ni katika umoja.

ambao umewakomboa

Yahwe kuwaokoa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri inazungumziwa kana kwamba Yahwe alilipa pesa kuwakomboa watu wake kutoka utumwani.

na usiweke hatia juu ya umwagaji damu usio na kosa miongoni mwa watu wako Israeli

Hii ni lahaja. "na usiwafanye watu wa Israeli kana kwamba wana hatia ya kuua mtu asiyekuwa na hatia"

Kisha umwagaji damu utasamehewa kwao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kisha Yahwe atasamehe watu wake Israeli kwa kifo cha mtu asiyekuwa na hatia"

utaweka mbali umwagaji damu usio na hatia miongoni mwenu

"hautakuwa na hatia tena kwa kuua mtu asiyekuwa na hatia"

yaliyo mema machoni pa Yahwe

Maneno "machoni pa Yahwe" ni lugha nyingine ya "kile Yahwe anachofikiri ni sahihi"