1.2 KiB
Ataamsha nguvu zake na moyo wake
Nguvu na moyo (ni ujasiri) vinaongelewa kana kwamba walikuwa ni watu ambao mtu fulani angeweza kuwaamsha ili watendo tendo.
moyo
Mahali hapa unawakilisha ujasiri
atapigana vita
"atapigana kinyume chake"
jeshi kubwa
"pamoja na jeshi kubwa ambalo atalikusanya"
hataweza kusimama
Kutokusimama kunawakilisha hali ya kushindwa.
wanaokula chakula chake kizuri
Hii inarejelea washauri wa mfalme. Ilikuwa na kawaida kwa washauri waliominiwa na mfalme kula chakula pamoja naye.
jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika,
Mahali hapa kushindwa kabisa kwa jeshi kunasemwa kana kwamba lilikuwa ni gharika la maji ambalo hulifutilia mbali.
wengi wao watauawa
Hii inarejelea kufa katika vita.
wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake
Mahali hapa neno "moyo" linawakilisha tamaa za mtu. Tamaa zinaongelewa kana kwamba kilikuwa ni kitu ambacho mtu anaweza kukiweka katika mkao fulani.
watakaa katika meza moja
Kukaa katika meza moja kuna maanisha kitendo cha kuongea pamoja na mtu mwingine.
haitakuwa na maana yoyote
"lakini mazungumzo yao hayatawasaidia"
Kwa kuwa mwisho utatokea katika kipindi ambacho kimeshapangwa
Hii inatuambia kwamba mkutano wao hautakuwa na mafanikio.