sw_tn/dan/11/20.md

1.2 KiB

mtu mwingine atainuka

Kuinuka katika nafasi ya mfalme inawakilisha kufanyika kuwa mfalme katika nafasiya mfalme aliyepita.

atamfanya mtoza ushuru apite

mtoza ushuru atapita katika nchi akiwalazimisha watu walipe kodi.

atakatiliwa mbali

Kiambishi 'a' kinamrejelea mfalme mpya. Kukatiliwa mbali ina maana ya kufa.

lakini si kwa hasira

Maana zinazokubalika 1) hakuna hata mmoja aliyekuwa na hasira na mfalme 2) tuko hilo na sababu ya kifo cha mfalme yalitunzwa kama siri.

mtu wa kudharauliwa ambaye watu hawatampa heshima ya nguvu ya kifalme

Watu watakataa kumheshimu kama mfalme kwasababu yeye si mzawa wa wafalme.

jeshi litafutiliwa mbali kama gharika

Kufutiliwa mbali kunawakilisha hali ya kuharibiwa. Hii pia yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji."jeshi lake litaangamiza kabisa jeshi kubwa kama gharika linavyoteketeza kila kitu katika njia yake"

Jeshi na kiongozi wa agano wataangamizwa wote kwa pamoja

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "ataliangamiza jeshi na kiongozi wa agano"

kiongozi wa agano

Kirai hiki kinamrejelea mtu alijawa na nafasi muhimu ya kidin ambayo Mungu anaihitaji katika agano, ambaye ni kuhani mkuu (ambaye aliuawa katika mwama 171 KK)