1.3 KiB
Maelezo ya jumla
Malaika anaendelea kuongea na Danieli.
Mfalme wa Kaskazini atakuja
Hapa "mfalme wa Kaskazini" anajumuisha na jeshi lake pia. "Jeshi la mfalmw wa Kaskazini litakuja"
kuizingira nchi kwa kuweka vilima
Hii inarejelea kitendo cha kurundika udongo ili wanajeshi waweza kuufikia urefu wa ukuta wa mji iili kuwashambulia. Wanajeshi na watumwa wataweka udongo kwenye vikapu na kuvibeba hadi mahali sahihi, na kuumwaga ili kuinua kilima cha udongo.
Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima
"Mfalme wa Kaskazini" hapa inamaanisha wanajeshi katika jeshi la mfalme, ambao wangefanya kazi halisi ya kutengeneza vilima vya udongo.
ngome
Kuta na vitu vingine vilivyojengwa ili kulinda mji
Hawatakuwa na nguvu za kusimama
Mahali hapa kitendo cha kusimama kinawakilisha uwezo wa kupigana.
yeye ajaye ataenenda kwa kufuata tamaa zake kinyume chake
"Mfalme atakayevamia atafanya kili kitu anachokitaka kinyume na mfalme mwingine."
Atasimama
Mahali hapa kusimama kuna maana ya kutawala
nchi ya uzuri
Hii inarejelea nchi ya Israeli . angalia ulivyotafsiri katika 8:9
uharibifu utakuwa mkononi wake
Mahali hapa "uharibifu" unawakilisha nguvu ya kuharibu. Pia, nguvu ya kuharibu inasemwa kana kwamba kilikuwa ni kitu ambacho mtu anaweza kukishikilia katika mikono yake.