sw_tn/dan/11/01.md

742 B

Maelezo ya jumla

Katika Danieli 11:1 hadi 12:4, yeye aliyekuwa akiongea na Danieli katika sura ya 10 anamwambia kile kilichoandikwa katika kitabu cha ukweli. Hiki ni kama kile alichosema angekifanya katika 10:20.

Katika mwaka wa kwanza wa Dario

Dario alikuwa ni Mfalme wa Umedi. "Mwaka wa kwanza" hurejelea mwaka wa kwanza ambao alikuwa Mfalme.

Wafalme watatu watainuka katika Uajemi,

"Wafalme watatu watatawala juu ya Uajemi"

na mfalme wa nne atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote

"baada yao mfalme wa nne atakuja kutawala ambaye atakuwa na fedha nyingi kuliko watatu waliomtangulia"

nguvu

Maana zinazoweza kukubalika ni 1)mamlaka au 2) nguvu za kijeshi

atamwamsha kila mtu

"atamsababisha kila mtu atake kupigana"