sw_tn/dan/09/24.md

1.5 KiB

Miaka sabini na saba zimeamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu

Mungu alitoa amri kwamba angefanya mambo kwa ajli ya watu na mji mtakatifu

Miaka sabini na saba...majuma saba na majuma sitini na mbili.

Hii si njia ya kawaida ya kuhesabu kwa Waisraeli. Kama itawezekana tafsiri kwa njia ambayo itatunza matumizi ya namba saba. "sabini mara miaka saba...saba mara miaka saba... sitini na mbila mara miaka saba"

watu wako na mji wako mtakatifu

Neno "wako" linamrejelea Danieli. Watu ni Waisraeli na mji mtakatifu ni Yerusalemu.

kukomesha hatia na kumaliza dhambi

Wazo limerudiwa ili kutia mkazo juu ya jinsi jambo hili litakavyotokea.

kutimiza maono

Hapa maneno 'kutimiza maono" ni nahau yenye maana ya kuhitimisha. "kukamilisha maono"

maono na unabii

Maneno haya katika muktadha huu yana maana moja. Yanatoa uhakika kwa Danieli kwamba maono ya Yeremia yalikuwa ni unabii kweli.

Ujue na kufahamu

Maneno haya yametumika kwa pamoja kuonesha na kuufanya umuhimu uwe wazi.

Mpakwa mafuta

Kutia mafuta ni tendo la ishara linaloonesha kwamba mtu fulani alichaguliwa. "Mtu yule ambaye Mungu anamtia mafuta"

kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili.

Haya yakiwekwa pamoja ni 69 kati ya 70 saba ilivyoongelewa ni 24.

Yerusalemu itajengwa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "watu wataijenga Yerusalemu"

handaki

ni shimo chini ya ardhi kuuzunguka mji au jengo, mara kwa mara huwa na maji ndani yake.

kwa nyakati za shida

"muda wa mateso makubwa"