sw_tn/dan/07/13.md

1.1 KiB

Maelezo ya jumla

Vifungu vingi vya mistari ya 9-14 ni lugha ya picha yenye mistari sambamba iliyo na maana sawa.

nilimwona mtu mmoja anakuja ... kama mwana wa mtu

Mtu ambaye Danieli alimwona hakuwa ni mtu wa kawaida, lakini alikuwa na mwonekano kama wa kibidamu. "Niliona usiku ule mtu fulani ambaye anafanana na na mwana wa mtu, yaani alikuwa na umbo la kibinadamu"

katika mawingu ya mbinguni

"pamoja na mawingu ya angani"

kwa Mzee wa Siku

Hii inamrejelea Mungu ambaye ni wa milele.

aliletwa mbele zake

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. 'walimleta huyu mwana wa mtu kwa Mzee wa Siku" au "alisimama mbele yake"

Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme

Maelezo haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Yeye aliyeonekana kama mwana wa mtu alipokea mamlaka ya kutawala, utukufu, na nguvu za kifalme."

nguvu za kifalme

Hii inarejelea "mamlaka"

hayatapita,..... hautaangamizwa

Virai hivi viwili vina maana ile ile

ule ambao hautaangamizwa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " kwamba hakuna hata mmoja atakayeangamiza"